Kwa mujibu wa gazeti la Al Ittihad, sherehe hiyo itafanyika chini ya usimamizi wa Sheikh Saud bin Sagar al Qasemi mtawala wa Ras al Khaimah katika Kituo cha Utamaduni cha Wizara ya Utamaduni, Vijana na Ustawi wa Jamii.
Sheikh ‘Omar bin Abdul Aziz Al-Qasemi katibu mkuu wa mashindano ya Qur'ani katika eneo hilo amesema awamu ya 12 ya mashindano ya Qur'ani ya Ras al Khaimah ilikuwa na washiriki 80. Ameongeza kuwa mashindano hayo yalijumuisha kuhifadhi Qur'ani kamili, juzuu 20, 10, 5 na 3 pamoja na tajwidi.
953898