Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina Ismail Hania amesema tangazo la mshikamano wa Wapalestina na Adnan Khidhr, mateka wa Kipalestina mbaye ameanza mgomo wa chakula tangu siku 62 zilizopita, ni ujumbe muhimu kwamba taifa la Palestina linashikamana na suala la kukomboa mateka wanaoshikiliwa katika korokoro za Israel.