IQNA

12:50 - February 20, 2012
Habari ID: 2277418

Mitazamo ya kisiasa na kijamii ya Imam Musa Sadr kuchunguzwa

Kikao cha kwanza cha vikao vilivyoandaliwa kuchunguza mitazamo ya kisiasa na kijamii ya Imam Musa Sadr kimepangwa kufanyika leo Jumatatu huko Beirut mji mkuu wa Lebanon.

Kikao hicho kilichopangwa kuanza leo saa nane alasiri kwa wakati wa Lebanon kimeandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Imam Musa Sadr mjini Tehran na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Beirut.
Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotazamiwa kushiriki kikao hicho ni Swadiq Nablosi, mwakilishi wa Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Jabal Amil nchini Lebanon na Talal Atrisi, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya Kisiasa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Masuala ya Kijamii kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Lebanon.
Vikao viingine vimepangwa kufanyika siku za Jumanne na Jumatano mjini Beirut.
Rima Fakhri, mtafiti wa masuala ya kisiasa ambaye pia ni mwanachama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, Affaf al-Hakim, Mkuu wa Kitengo cha Wanawake cha Hizbullah na Hussein Rihal, Mkuu wa Kitengo cha Upashaji Habari cha Hizbullah ni shakhsia wengine muhimu waliopangiwa kuzungumza katika kikao hicho. 956016
captcha