IQNA

Hamid Karzai asisitiza kuadhibiwa waliochoma moto Qur'ani Tukufu

14:24 - February 27, 2012
Habari ID: 2281555
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amewaomba wananchi wa nchi hiyo wawe watulivu kuhusiana na kitendo kiovu cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu kilichofanywa na askari wa Marekani na kwa mara nyingine ametoa wito wa kuadhibiwa wahalifu wote waliohusika na tukio hilo ka kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Waislamu.
Maandamano makubwa yamekuwa yakifanyika katika miji tofauti ya Afghanistan kufuatia kitendo hicho cha dharau cha askari wa Marekani dhidi ya Qur'ani Tukufu, jambo ambalo limemfanya Rais Karzai awaombe wananchi wa nchi hiyo wawe na subira na utulivu na kutoruhusu maadui kutumia suala hilo kufikia malengo yao.
Amesema wanapasa kutowaruhusu maadui wa utulivu na amani ya Afghanistan kutumia fursa hiyo kwa lengo la kupora utajiri wa nchi hiyo.
Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wananchi wa Afghanistan kufuatia kitendo cha askari wa Marekani walio katika kituo cha anga cha Bagram kuchoma moto Qur'ani Tukufu. 961095
captcha