IQNA

Ramani ya Muirani ya kupamba Makka yashinda

13:49 - March 12, 2012
Habari ID: 2290331
Msanifu majengo wa Iran ameibuka mshindi katika mashindano ya kimataifa ya 'Kuifanya Makka iwe Maridadi' yaliyoandaliwa na Saudi Arabia kwa lengo la kuuboresha mji mtakatifu zaidi katika Uislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wasanifu majengo kutoka nchi 24 walishiriki katika mashindano hayo na waliwasilisha ramani 442 ambapo mpango wa msanifu majengo Muirani umepata nafasi ya kwanza.
Msanifu majengo Muirani Mohammad Ridha Karbaschi kutoka Kashan amekuwa wa kwanza baada ya pendekezo lake kuchunguzwa na jopo la majaji wa kimataifa. Ramani ya Muirani huyo itatumika katika mpango wa 'Kupamba Mji Mtakatifu wa Makka' hivi karibuni.
Mohammad Ridha Karabaschi ametunukiwa zawadi ya dola elfu 30 na kamati ya mashindano hayo.
970100
captcha