Katika maandamano hayo wananchi wametangaza bayana kwamba watapinga katiba yoyote itakayopitishwa pasina kuwepo sheria za Kiislamu ndani yake. Waandamanaji wametoa nara kama vile, 'Wananchi wanataka sheria za Mwenyezi Mungu zitekelezwe' na 'Tunisia ni nchi ya Kiislamu'. Aidha makundi zaidi 200 ya kisiasa na kiraia yametia saini taarifa ya kutaka sheria za Kiislamu zitekelezwe nchini humo.
Bunge la Waasisi la Tunisia liko katika mkakati wa kuandika katiba mpya ya nchi hiyo. Zoezi la kuandika katiba hiyo linatazamiwa kumalizika katikati ya mwaka huu wa 2012.
Utawala wa kiimla wa Tunisia ulipinduliwa Januari 14 mwaka 2011 kufuatia mwamko wa Kiislamu wa wananchi. Dikteta wa Tunisia aliyetimuliwa madarakani Zine el Abidine Ben Ali amepewa hifadhi na utawala wa Saudi Arabia.
973109