Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kuwa Syria inaandamwa na madola ya Magharibi pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu kutokana na misimamo yake ya kuunga mkono mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel. Ayatullah Khatami amezionya nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia akisema kuwa moto wanaojaribu kuuwasha huko Syria utakuwa kama mtego wa panya ambao hunasa waliokuwemo na wasiokuwemo.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran aidha amekumbusha kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu zinaisakama Syria ili kupoza moto unaowaka katika nchi zao lakini amesisitiza kuwa mwamko wa Kiislamu utawafagia madikteta wote katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa kiarabu kwa ujumla.
Vilevile amekosoa hatua ya nchi za Kiarabu ya kupuuza mauaji na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa kifalme wa Bahrain dhidi ya raia wa nchi hiyo na kulaani uvamizi wa Saudi Arabia ambayo imetuma majeshi huko Bahrain kukandamiza wananchi wa nchi hiyo.
979335