IQNA

Kikokotoo (Calculator) cha wakati wa Sala katika safari za ndege

14:58 - April 09, 2012
Habari ID: 2300825
Kikokotoo (Calculator) cha kwanza duniani cha kuwawezesha Waislamu kufahami wakati wa sala katika safari ndani ya ndege kimezinduliwa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kikokotoo (Calculator) cha wakati wa sala katika safari za ndege (Air Travel Prayer Time Calculator) kimezinduliwa na shirika la Crescentrating nchini Singapore. Shirika hilo pia linahusika na masuala ya kuainisha hoteli halali na masuala mengine ya safari yanayohusiana na Waislamu.
Chombo hicho kinatumia data kuhusu nyakati za sala sehemu ilipoanzia safari na sehemu itakaposhuka ndege na pia nyakati za sala katika njia itakayotumiwa na ndege na kisha kutumia algorithm kuainisha wakati halisi wa sala katika safari ya ndege.
Hivi sasa Waislamu wanaosali ndani ya ndege hutegemea wakati wa sala ardhini jambo ambalo huwachanganya wengi. Baadhi ya wanazuoni hupendekeza kuwa wasafiri wa ndege waainishe wakati wa sala kwa kutegemea eneo walikotoka au wanakoelekea huki wengine wakisisitiza kuwa wakati wa mchana wasafari waangalie sehemu ya jua angani.
Lakini sasa baada ya kuzinduliwa Kikokotoo (Calculator) cha wakati wa Sala katika safari za ndege wasafiri Waislamu wanaweza kutembelea tovuti ya crescentrating.com na kufuata maagizo wanaweza kupata wakati halisi wa sala katika safari.
981577
captcha