IQNA

Ahmadinejad asema Iran imesimama kidete mbele ya mabeberu

17:19 - April 17, 2012
Habari ID: 2306824
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika sherehe za Siku ya Jeshi kuwa taifa la Iran limesimama kidete mbele ya mabeberu wote huku likilinda haki zake zote na za wanaodhulumiwa, kwa kuungwa mkono na vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Iran.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo leo mjini Tehran katika sherehe za Siku ya Jeshi liyofanyika kando kando ya Haram ya Imam Khomeini MA na mbele ya hadhara ya makamanda wa vikosi vya kijeshi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah pamoja na wawakilishi wa kijeshi wa kigeni waliopo hapa Tehran. Ameongeza kuwa, jeshi la Iran linamtegemea Mwenyezi Mungu na wananchi wake waumini na kwamba jeshi la aina hiyo haliwezi kushindwa mbele ya mabeberu.
Sambamba na kubainisha kwamba hii leo mabepari wa dunia wasio na ustaarabu na wenye kujiona wanafanya kila wawezalo ili kuwakandamiza wapigania uhuru na uadilifu na mataifa yanayotaka kujitegemea duniani, Dakta Ahmadinejad ameongeza kuwa, ni jambo lililo wazi kuwa waistikbari hao wanapinga vikali vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Iran na wana woga na wahka juu ya kuweko jeshi la Iran lenye heshima na imara.
captcha