Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema serikali ya Marekani ni mshirika katika kuvunjiwa heshima Qur'ani na amehoji ni kwa nini Wamarekani ambao hawawezi hata kustahamili mjadala kuhusu maudhui ya 'Holocaust' wanavunjia heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu duniani?
Ayatullah Khatami pia amekosoa kimya cha Wakristo duniani kufuatia hatua ya kasisi Mkristo Marekani kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Kuhusu uchaguzi ujao wa rais nchini Misri, Ayatullah Khatami amesema taifa lililostaarabika la Misri halitaruhusu mapinduzi ya wananchi yatekwe. Ameongeza kuwa waliohudumu katika utawala wa dikteta Mubarak hawapasi kuchaguliwa na kuongeza kuwa Wamisri watamchagua rais anayepinga ubeberu na Uzayuni.
Kuhusu kadhia ya Bahrain, Ayatullah Khatami amesema kuwa, taifa la Iran litaunga mkono taifa linalodhulimiwa la Bahrain kama linavyounga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.
999654