IQNA

As Sahifat ul Kamila as Sajjadiya kwa lugha ya Kiswahili

12:33 - May 14, 2012
Habari ID: 2325469
Tarjuma ya Kiswahili ya As Sahifat ul Kamila as Sajjadiya imetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili na Taasisi ya Al Itrah ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti katika tovuti ya ibn-tv.com, as-Sahifat-ul-Kamilah as-Sajjadiyyah kitabu cha dua cha Imam Zainul Abideen AS kimetarjumiwa ili kwa mara ya kwanza ili kuwanufaisha watu wanaozungumza lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa mujibu wa taasisi ya Al Itrah kitabu hicho cha dua kimetarjumiwa na Sheikh Haroon Pingili na kuhaririwa na Al Haji Hemedi Lubumba Selemani na Dk. Ja'afar Tijani.

Taasisi ya Al Itrah yenye makao yake katika mji mkuu wa Tanzania Dar-es-Salaam inajihusisha na kuchapisha vitabu kuhusu mafundishoo ya Kiislamu kwa mtazamo wa Ahul Bayt AS.
1005996
captcha