IQNA

18:01 - May 21, 2012
Habari ID: 2330986

Wanachuo wa Burkina Faso walalamikia marufuku ya hijabu

Wanachuo wa Kiislamu wa Burkina Faso wamemwandikia barua Waziri wa Masula ya Kijamii wa nchi hiyo wakilalamikia tabia ya baadhi ya wasimamizi wa masomo nchini humo ya kuwazuia wanachuo wa kike wanaovalia vazi la hijabu, kushiriki katika vikao vya mitihani.

Kwa mujibu wa tovuti ya lefao, wanachuo hao wamesema katika barua hiyo kwamba licha ya kuwepo uhuru wa kujieleza na mavazi nchini Burkina Faso lakini inaonekana kuwa mavazi ya Kiislamu yamekuwa yakiwakera baadhi ya watu walio na chuki na Uislamu nchini humo kiasi kwamba baadhi ya wasimamizi wa masomo wamekuwa wakiwazuia wanachuo wa Kiislamu wanaovalia hijabu kushiriki vikao vya mitihani nchini. Barua hiyo inasema, licha ya kuwa mavazi hayo ya Kiislamu ni ya kawaida kabisa kiasi kwamba hayazuii kubainika utambulisho wa wanachuo na wanafunzi wa kike wanaovalia hijabu, lakini baadhi ya wasimamizi na maafisa wa wizara ya elimu wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na kuwazuia wanafunzi na wanachuo kushiriki kwenye vikao vya mitihani. Wanachuo hao wanasema hatua hiyo ni ukiukaji wa wazi wa haki za wanawake wa Kiislamu na ubaguzi dhidi ya raia wa Burkina Faso na kwa hivyo wameitaka Wizara ya Masuala ya Kijamii kuchukua hata zinazofaa kwa lengo la kukabiliana na wakiukaji wa katiba ya nchi hiyo. 1012823
captcha