IQNA

12:32 - June 06, 2012
Habari ID: 2341072

Mataifa ya eneo yamepata ilhamu kutoka fikra za Imam Khomeini MA

Mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Ikwanul Muslimin ya Misri amesema watu ambao wameamka kupinga dhulma na kuangisha tawala za kidikteta katika nchi kama vile Tunisia na Misri wamepata ilhamu kutoka fikra za Imam Khomeini MA.

Akizungumza Jumatatu katika kongamano la kimataifa lenye anuani ya 'Imam Khomeini na Sera za Kigeni, Kamal Halbawi ameongeza kuwa Imam Khomeini MA alikuwa shakhsia mkubwa ambaye alibadilisha mkondo wa historia na kuathiri siasa katika uga wa kitaifa na kimataifa.
Ameongeza kuwa Imam Khomeini MA alitekeleza madundisho ya mitume wa Allah SWT na alilipa kipaumbele suala la kupinga dhulma.
'Imam Khomeini MA alisisitiza umuhimu wa Waislamu kusimama kidete dhidi ya dhulma ambapo alifadhilisha kifo cha heshima kulika kuishi chini ya dhulma.'
Mwanaharakati huyo wa kisiasa Misri amesema hayati Imam Khomeini alitetea suala la umoja katika Ummah wa Kiislamu.
Aidha ameashiria hatua ya Imam Khomeini MA ya kutangaza Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds na kuongeza kuwa mbegu hiyo iliyopandwa katika siku za awali za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu sasa ni mti wenye nguvu na kila mwaka katika Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislamu hujitokeza na kutoa nara za kuunga mkono haki za Wapalestina.
Kongamano la kimataifa la 'Imam Khomeini na Sera za Kigeni' liliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.
1023232
captcha