IQNA

Maadhimisho ya Siku ya Karbala katika sherehe za kuzaliwa Imam Hussein (as)

18:23 - June 10, 2012
Habari ID: 2343724
Maadhimisho ya Siku ya Karbala yatafanyika tarehe 23 Juni sambamba na kufanyika sherehe za uzawa wa Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq.
Kwa mujibu wa tovuti ya Swautil Iraq, maonyesho ya pili ya kimataifa ya Karbala ni miongoni mwa ratiba maalumu zitakazotekelezwa katika siku hiyo ya Karbala ambapo mashirika muhimu ya kimataifa ya viwanda yapatayo 40 yatashiriki. Maonyesho hayo yatakayoanza tarehe 22 Juni yataendelea kwa muda wa siku nne. Mashirika yatakayoshiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na ya Uingerea, Italia, Russia, China na India. 1026437
captcha