Akibainisha suala hilo, Twahir Qadiri, mkuu wa taasisi hiyo amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa lengo la kueneza mafundisho ya Qur'ani katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Amesema mafunzo hayo yatatolewa katika maeneo ya vijijini hadi miji mikubwa kwa lengo la kuwafundisha wakazi wa maeneo hayo mafundisho muhimu ya kitabu hicho cha mbinguni.
Allama Afdhal Qadir kiongozi mwingine wa taasisi ya Minhajul Qur'an amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa madhumuni ya kuwashajiisha watu kujifunza Qur'ani Tukufu (saw). 1034079