Hayo yamesemwa na Nuh Ali Mar'i mwakilishi wa Lebanon katika Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran katika kitengo cha hifdhi ya Qur'ani nzima. Ameongeza kuwa anashiriki katika mashindano ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara ya kwanza na kabla ya mashindano haya alishiriki katika mashindano ya kitaifa ya Lebanon.
Amesema: "Nilikuwa na woga wa kupanda kwenye meza ya mashindano ya Qur'ani kwenye ukumbi wa mashindano haya na nilikuwa nikiamini kwamba ni vyema kuwatahini washiriki katika vyumba tofauti; lakini baada ya kuingia kwenye mashindano haya yanayoendeshwa kwa mbinu bora na mapokezi mazuri ya watayarishaji wake nimeondokewa na woga na kupata moyo."
Kuhusu jinsi alivyohifadhi Qur'ani Nuh Ali Mar'i amesema Jumuiya ya Qur'ani ya Lebanon imekuwa ikitayarisha mafunzo ya Qur'ani Tukufu na sherehe mbalimbali za kidini na pia masomo ya kitaalamu ya hifdhi ya Qur'ani ambayo hotolewa kila mwaka, na kwamba yeye mwenyewe ameweza kuhifadhi Qur'ani kupitia jumuiya hiyo.
Amesema kuwa alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 9 na aliweza kuhifadhi Qur'ani nzima akiwa na umri wa miaka 12. Amesisitiza kuwa kiwango cha mashindano ya sasa ya Qur'ani ya Tehran ni kizuri mno na huduma bora kabisa zinatolewa kwa washiriki. 1034095