IQNA

Tolea la 21 la Jarida la Mashia wa Mali latolewa

14:28 - June 23, 2012
Habari ID: 2352259
Toleo la 21 la jarida la Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Mali linaloitwa Sakina-Ashura lilichapishwa siku ya Alkhamisi.
Akibainisha suala hilo, Ahmad Diyalo mkuu wa Jumuiya ya Mashia wa Mali amesema jarida hilo ambalo huchapishwa katika kurasa nane huchapishwa kwa lugha ya Kifaransa.
Masuala mengi yakiwemo yanayozungumzia mwezi mtukufu wa Shaaban ambao ni mwezi wa Mtume Mtukufu (saw), njia za kupambana na ugaidi, Maimamu watoharifu (as) katika hadithi za Masuni, maswali 19 aliyomuuliza Imam Swadiq (as) tabibu wa Kihindi, semi za Imam Khomeini (as), amali maalumu za nusu ya mwezi wa Shaaban pamoja na fadhila za mwezi huu mtukufu ni baadhi ya mambo yaliyochapishwa kwenye jarida hilo.
Diyalo amesema kuwa jarida hilo ndilo la pekee linalodhaminiwa na wanafunzi wanaofuata madhehebu ya Ahlul Beit (as) nchini Mali. 1035325
captcha