Msafara huo ambao unajumuisha makarii, mahufadhi, wahadhiri, walimu na wakurugenzi wa taasisi za Qur'ani nchini Iran umetembelea sehemu tofauti za msikiti huo na kujifunza mengi kuhusiana nao. Msafara huo pia siku ya Jumatano ulitemebelea misikiti na maeneo mengine ya kihistoria katika mji huo ikiwemo misikiti ya Quba, Qiblatein, Fath, Shajara na makaburi ya mashahidi wa vita vya Uhud.
Msafara huo pia umetembelea kituo cha mahujaji wa Kiirani mjini humo ambapo Muhammad Ansari, Mshauri wa Kituo cha Uratibu, Uenezaji na Shughuli za Qur'ani cha Iran ametoa ripoti kuhusu safari ya msafara wa kwanza wa wanaharakati hao wa Qur'ani katika ardhi hiyo ya wahyi.
Mashindano ya Qur'ani na kasida ni baadhi ya ratiba zilizotekelezwa katika safari ya msafara huo wa Iran katika mji mtakatifu wa Madina. 1035248