IQNA

Kongamano la kutaamali Qur'ani lafanyika India

14:38 - June 23, 2012
Habari ID: 2352264
Kongamano la kutafakari na kutaamali Qur'ani Tukufu limefanyika katika mji wa Bareli katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
Kongamano hilo lilifanyika siku ya Jumatano ambapo wanazuoni, wataalamu wa kidini na Qur'ani pamoja na makarii mashuhuri wa Qur'ani wa India walihudhuria.
Washiriki waliozungumza katika kongamano hilo waligusia mafundisho muhimu ya kitabu hicho kitakatifu na kusisitiza kwamba yanamuokoa mwanadamu kutokana na mambo mengi yanayomuhatarisha maishani na kumdhaminia saada huko Akhera. Wamesema taaluma na maenedeleo makubwa ambayo hivi sasa yamepatikana duniani yamezungumziwa katika kitabu hicho cha mbinguni lakini kwa bahati mbaya Waislamu hawazingatii kwa kina mafundisho yake.
Wamesema kwa masikitiko kwamba Waislamu wengi hawazingatii mafundisho muhimu ya kitabu hicho wala kutafakari yaliyomo bali hutosheka tu kwa kukisoma juu juu. 1035258
captcha