IQNA

Tiba ya Qur’ani na Kiislamu yafunzwa katika vyuo vikuu Iran

14:36 - June 23, 2012
Habari ID: 2352324
Masomo ya tiba ya Qur’ani na Kiislamu yanafunzwa kinadharia na kivitendo katika vyuo vikuu vya tiba vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vinavyosimamiwa na Wizara ya Afya na Elimu ya Tiba.
Akizungumza na mwandishi wa IQNA, Waziri wa Afya Daktari Bi. Mardhia Wahid Dastjerdi amesema mbali na mafunzo hayo pia kumekuwepo na semina na vikao mbalimbali vya kielimu na kisayansi kuhusu tiba ya Qur’ani na Kiislamu.
Ameongeza kuwa nchini Iran kumezinduliwa vituo kadhaa maalumu vya tiba ya Qur’ani na Kiislamu ili kuhakikisha kuwa tiba hiyo inatekelezwa ipasavyo kote nchini.
‘Mafundisho ya Kiislamu yana nafasi muhimu katika kustawisha moyo wa kibinadamu na kujitolea mhanga miongoni mwa wananchi,’ amesema huku akiashiria idadi kubwa ya wananchi wa Iran ambao wanatoa damu kwa wale wanaohitajia.
Amesema kutokana na moyo wa Wairani kujitolea katika kuwapa damu wanaohitajia, hivi sasa, Alhamdulillah, Iran haihitajii damu kutoka nje ya nchi isipokuwa katika kesi nadra kama albumin ambayo ni proteni ya damu.
1030937
captcha