IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran ni moja ya matukio muhimu ya Qur'ani duniani

15:55 - June 27, 2012
Habari ID: 2354818
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoandaliwa mjini Tehran ni moja ya matukio muhimu ya Qur'ani duniani.
Hayo yamesemwa na Rashid Muahmmad Swaleh kutoka mjini Mombasa Kenya, ambaye ni mmoja wa washiriki wa mashindano ya Qur'ani yaliyomalizika hivi karibuni mjini Tehran.
Mshiriki huyo aliyewakilisha Kenya katika mashindano hayo amesema mashindano hayo ya 29 yalifanyika kwa kiwango cha juu kabisa. Amesema kwa kushiriki katika mashindano hayo, amepata kufahamu kwamba Qur'ani Tukufu inapewa umuhimu mkubwa na maalumu nchini Iran.
Mshiriki huyo aliyeshiriki katika kitengo cha kiraa katika mashindano hayo amesema kila Mwislamu anapasa kusoma, kuzingatia na kutekeleza maishani mafundisho ya kitabu hicho cha mbinguni. Ameendelea kusema kuwa Waislamu wanapasa kutumia mafunzo ya kitabu hicho kuimarisha umoja na udugu miongoni mwao la sivyo watakabiliwa na matatizo makubwa maishani.
Rashid Muahmmad Swaleh amesema kuandaliwa kwa mashindano kama hayo ya Tehran kuna athari kubwa katika kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu.
Amesema atakapowasili nchini kwake atawasihi wahusika kuandaa mashindano kama hayo nchini humo. 1037921
captcha