IQNA

Mashindano ya kimataifa ya 'Nusratul Qur'an' kuanza Iraq kesho

15:57 - June 27, 2012
Habari ID: 2354819
Waandaaji wa duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iraq yaliyopewa jina la Nusratul Qur'ani wamesema mashindano hayo yataanza katika mji mkuu wa nchi hiyo hapo leo Jumatano.
Sheikh Mazin as-Saidi, Mkuu wa Jumuiya ya Qur'ani inayofungamana na Taasisi ya Shahid Sadr wa Pili na anayesimamia mashindano hayo amesema mashindano hayo ya kimataifa yatazishirikisha nchi 26 za Kiarabu na Kiislamu.
Amesema kuongezeka kwa idadi ya nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo kunabainisha wazi kuboreka kwa kiwango chake.
Sheikh Mazin as-Saidi amesema duru ya kwanza ya mashindano hayo iliyofanyika katika mwezi mtukufu wa Shaaban mwaka uliopita ilizishirikisha nchi 16. 1038371
captcha