IQNA

Hafidh wa Kenya: Iran inastahiki pongezi kwa kuiheshimu Qur'ani

16:12 - June 27, 2012
Habari ID: 2354902
Hafidh wa Qur'ani kutoka Mombasa Kenya Abdulqadir Yusuf aliyeshiriki Mashidano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Iran amesema kile ambacho kimemuathiri ni namna watu wa Iran wanavyoiheshimu sana Qur’ani Tukufu.
Katika mahojiano na IQNA, amesema, ' kwa hakika nchini Iran Qur'ani Tukufu inapewa umuhimu mkubwa. Kati ya mambo niliyoamua ni kuwa nikirejea Kenya nitawafahamisha Waislamu kuhusu hadhi kubwa iliyopewa Qurani hapa Iran na ulazima wa sisi kufuata mfano wa Wairani.'
Ameongeza kuwa watu wa Iran wamepata maendeleo na mshikamano kwa ajili ya Qur’ani na hili ni jambo muhimu.
Kuhusiana na nafasi ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Iran katika kuimarisha umoja wa Waislamu amesema: 'Hii ni nukta muhimu kwani kushiriki idadi kubwa ya Waislamu ni jambo ambalo bila shaka litazidisha Umoja wa Kiislamu na kukurubisha madhehebu ya Kiislamu. Mimi binafsi nilikuwa sidhani kuna Waislamu wanaoweza kusoma Qur’ani katika baadhi ya nchi za Ulaya lakini nilipokuja hapa nimeshangaa kuona maqarii na mahafidh kutoka nchi mbalimbali za dunia. Imekuwa fursa nzuri na tunaishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwaleta pamoja Waislamu.'
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Iran yalianza Tehran tarehe 27 Rajab ( 17 Juni) kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kubaathiwa Mtume SAW na kuendelea hadi tarehe mbili Shaaban sawa na 22 Juni. Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 100 kutoka nchi 65 za Kiislamu za zisizokuwa za Kiislamu.
1037969
captcha