Katibu wa mashindano ya Nusratul Qur'an Sheikh Mazin al Saidi amesema kuwa mashindano hayo yaliwakutanisha pamoja washindani kutoka nchi 26 za Kiarabu na Kiislamu na yalimalizika jana tarehe 29 Juni.
Amesema wasomaji wawili kutoka Iran wameshika nafasi za kwanza katika hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu. Amesema Shujaa Zuwaidat ameshika nafasi ya kwanza katika kitengo cha kiraa na Sayyid Jawad Hussaini ameshika nafasi ya kwanza katika hifdhi ya Qur'ani nzima.
Al Saidi amesema kuwa duru ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iraq ilifanyika mwezi Shaaban mwaka jana ikiwashirikisha wasomaji kutoka nchi 16. 1041150