Waandaaji wa mashindano hayo wamesema kuwa kutokana na ukweli kuwa adhana ni sehemu muhimu ya nembo za ulimwengu wa Kiislamu kuna haja ya kusomwa adhana hiyo kwa sauti ya kuvutia na kwa kufuata kanuni na misingi inayokubalika.
Kwa msingi huo kila mwaka Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki huandaa mashindano maalumu ya wasomaji adhana ambapo mwaka huu hatua ya mwisho ya mashindano hayo imefanyika katika mji wa Alaziq.
Washindani 10 bora walichaguliwa kushiriki katika mashindano hayo ambapo washindi wa mwisho walichaguliwa na waamuzi na kutunukiwa zawadi. Mashindano hayo huwavutia Waturuki wengi kila mwaka. 1041853