Viongozi wa masuala ya kiutamaduni na kidini, mahafidh na makarii wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu wameshiriki katika mahafali hiyo muhimu.
Mahafidhi na makarii wa kitaifa na kimataifa walioshiriki mahafali hiyo waliwafariji washiriki kwa kuwasomea aya kadhaa za Qur'ani kwa mahadhi na sauti za kuvutia.
Ikiwa ni katika ratiba za mahafali hiyo washiriki wawili waliwavutia sana hadhirina kwa kuadhini adhana kwa wakati mmoja na kwa sauti nzuri za kuvutia.
Mahafali hiyo ilifanyika Jumamosi tarehe 30 Juni ambapo wasomaji na mahafidh bora wa Qur'ani walishukuriwa na kutunukiwa zawadi. 1042191