IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Misri

13:08 - July 02, 2012
Habari ID: 2359118
Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Al Azhar Misri ya vijana walio chini ya umri wa miaka 25 yataanza 19 hadi 26 Ramadan 1433 (7-14 Agosti 2012).
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Awqaf ya Misri na yanalenga kuwahimiza vijana kuhifadhi Qur’ani na kutekeleza mafundisho yake katika maisha yao ya kila siku.
Mashindano hayo yatakuwa na vitengo vya kuhifadhi Qu’rani kikamilifu, tajweed, tarteel na tafsiri ya Juzuu ya 15 ya Qur’ani, kuhifadhi juzuu 20 na kuhifadhi juzuu sita.
Washiriki wanapaswa kuwa na ufahamu wa kiwango cha juu kuhusu kuhifadhi Qu’rani.
1042823
captcha