IQNA

Darsa za Qur'ani Tukufu kutolewa mjini London

17:31 - July 03, 2012
Habari ID: 2360036
Masomo ya muda mfupi ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kutolewa katika mtaa wa Edmonton nchini Uingereza kwa kipindi cha siku nne katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa tovuti ya ijma, masomo hayo ambayo yamedhaminiwa na Kituo cha Kiislamu cha London yatatolewa tarehe 8, 9, 15 na 16 za mwezi mtukufu wa Ramadhani tokea saa 4 hadi 12 jioni za Uingereza.
Katika masomo hayo maana jumla ya sura 114 za Qur'ani itabainishwa na wanazuoni wanne mashuhuri wa London.
Matatizo ya kutarjumiwa Qur'ani katika lugha nyingine zisizokuwa Kiarabu, ujumbe jumla wa sura na masomo tunayopata kutokana na kila sura ni baadhi ya mambo yatakayochunguzwa katika masomo hayo. 1043445
captcha