IQNA

Sherehe za uzawa wa Imam Mahdi (af) zafanyika Tanzania

6:30 - July 05, 2012
Habari ID: 2361296
Sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa Imam Mahdi (af) zilifanyika jana Jumatano huko Dar es Salaam, Tanzania.
Sherehe hizo zilianza jioni mara tu baada ya kumalizika swala za Magarib na Isha. Wahadhrii na wasomi wa Kiislamu wa Tanzania walishiriki katika sherehe hizo na kutoa hutuba mbalimbali kuhusiana na fadhila za nusu ya mwezi mtukufu wa Shaaban na sababu za kughibu Imam Mahdi (af) pamoja na majukumu ya Waislamu wanaosubiri kudhihiri kwa mtukufu huyo.
Mashairi kuhusu fadhila na maadili ya Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) na hasa Imam Mahdi Muahidiwa (af) ilikuwa sehemu ya ratiba za sherehe hizo.
Matabaka ya wafuasi na wapenzi wa Ahlul Bait (as) wakaazi wa Dar es Salaam walialikwa katika sherehe hizo muhimu. 1044483
captcha