Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ingawa Finland haina vyuo vya juu vya Kiislamu lakini kuna madrasa nyingi zisizo rasmi katika maeneo yenye Waislamu wengi. Ingawa wakuu wa Finland hawatangazi idadi ya Waislamu nchini humo lakini Profesa Jaakko Hämeen-Anttila anakadiria idadi hiyo kuwa arobaini elfu.
Kituo cha Kiislamu Helsinki ni kati ya maeneo ambayo Waislamu nchini humo wanajifunza Qur’ani.
Yunus Ali mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akihudhuria darsa za Qur’ani katika kituo hicho na anasema hivi, ‘awali masomo yalikuwa magumo kutokana na kujifunza Kiarabu, lugha ambayo inatafautiana na Kifini.’
Mwanafunzi mwenzake Muhammad Ahmad mwenye umri wa miaka 20 anasema alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri wa miaka saba. ‘Masomo ya Qur’ani kawaida huanzia nyumbani pale wazazi wanapowafundisha watoto wao’, anasema Ahmad ambaye sasa yuko katika chuo cha kujifunza uuguzi.
Ali na Ahmad wanasema Qur’ani ndio nuru inayowaongoza katika maisha yao ya kila siku.
1049192