IQNA

Iran, mbeba bendera ya harakati za Qur’ani duniani

14:07 - July 11, 2012
Habari ID: 2366020
Hivi sasa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio inayoongoza katika harakati za Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu, amesema mbunge mmoja wa Iran.
Akizungumza katika sherehe za kufungua Kongamano la Nne la Qur’ani na Wanawake mjini Tehran Julai 10, Bi Laleh Iftikhari ameashiria Kongamano la Kimataifa la Wanawake na Mwamko wa Kiislamu ambalo liNAfanyika Iran KWA sasa na kumesema kati ya washiriki 1000 kulikuwa wanaharakati na wataalamu wa Qur’ani kutoka nchi 88 duniani ambao wamejadili masuala ya Qur’ani na Mwamko wa Kiislamu.
Bi. Iftikhari amesema wanaharakati wa Qur’ani wamesema kongamano la Wanawake na Mwamko wa Kiislamu ni tukio la aina yake katika historia ya Waislamu duniani.
Bi. Iftikhari ambaye pia ni Mkuu wa Tume ya Qur’ani na Etrat katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) amesisitiza kuwa wanawake katika Ulimwengu wa Kiislamu wana jukumu maalumu la kulea kizazi cha Qur’ani. ‘Ili kutekeleza wajibu huu, wanawake wanahitaji wenyewe binafsi kuwa na tabia na mwenendo wa Qur’ani na wa Kiislamu’, ameongeza.
Mbunge huyo amesema Mtume Muhammad SAW ni kigezo kwetu kwani alikuwa na maadili bora ya Qur’ani. ‘Sisi pia tunapaswa kufuata maadili bora ya Qur’ani ili kujenga jamii ya Qur’ani na ya Kiislamu’, amesisitiza.
Bi. Iftikhari ameashiria kuwa tuko katika Mwezi wa Shaaban utakaofuatiwa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hivyo Waislamu wanapaswa kunufaika kikamilifu na fadhila za miezi hii miwili.
1049347
captcha