Sherehe hizo zilihudhuriwa na wafanyakazi wa ubalozi, Wairani wanaoishi mjini Paris pamoja na wapenzi wengine wa Ahlul Beit (as) mjini humo.
Akizunguza katika sherehe hizo Mishkaat Dini alizungumzia amali zinazopaswa kutekelezwa katika siku hizi tukufu na kisha kuchambua kwa undani nafasi ya mwanadamu mkamilifu katika Qur'ani Tukufu.
Mwishoni mwa sherehe hizo wageni walialikwa kwa karamu maalumu na kisha kuzawadiwa vifurushi vya bidhaa za kiutamaduni. 1050455