Shahrokh Faryusufi msanii mashuhuri wa Iran anatazamiwa kuonyesha kazi zake katika maonyesho hayo ambayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Utamaduni na Sanaa ya Qatar.
Kazi muhimu 30 za waandishi wa Qur'ani zinatazamiwa kuonyeshwa katika maonyesho hayo ya maandishi ya mkono ya aya za Qur'ani Tukufu ambayo yamepangwa kuendelea kwa muda wa wiki moja.
Maonyesho hayo yamepangwa kuanza sambamba na kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani. 1055056