Maktaba ya umma ya Fatma az-Zahra (as) inayofungamana na msikiti mkuu wa Imam wa Zama, yaani Imam Mahdi (af) imefunguliwa katika mtaa wa Pule Khushk katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Wanazuoni, walimu, wahadhiri na wabunge kadhaa wa Afghanistan wamehudhuria sherehe ya ufunguzi wa maktaba hiyo.
Maktanba hiyo ambayo ina ukubwa wa mita mraba 100 ina vitabu vingi na vifaa vya kisasa vinavyomwezesha msomaji kujishughulisha na masuala tofauti ya utafiti wa kielimu. Pia ina vivutio vingi vinavyowashawishi vijana kujishughulisha na usomaji kwa ajili ya kuinua viwango vyao vya kielimu na kiutamaduni.
Tunakumbusha hapa kwamba msikiti mkuu wa Imam Zaman (as) ni mmoja kati ya misikiti muhimu ya Afghanistan inayojishughulisha na masuala tofauti ya kiutamaduni, kidini na kielimu kwa manufaa ya matabaka tofauti ya jamii ya nchi hiyo na hasa tabaka la vijana. 1056069