IQNA

14:52 - July 21, 2012
Habari ID: 2373783

Ismail Hania: Mwamko wa Kiislamu utapelekea kukombolewa Palestina

Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesema kuwa, Mwamko wa Kiislamu na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu, yatapelekea kukombolewa ardhi za Palestina na Quds Tukufu.

Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesema kuwa, mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu yatapelekea kukombolewa ardhi za Palestina na Quds Tukufu.
Ismail Hania amesisitiza kwamba, wimbi la mapinduzi ya wananchi litaendelea kutanda mpaka pale umma wa Kiislamu utakapofanikiwa kung'oa mizizi ya ukoloni katika Mashariki ya Kati na kukombolewa Palestina na Baytul Muqaddas.
Hania ameongeza kuwa dikteta wa zamani wa Misri Hosni Mubarak alishirikiana na utawala wa Kizayuni katika kuliwekea mzingiro eneo la Ghaza.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hatua za ukandamizaji na kero katika msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu. Hatu hizo za Wazayuni zimekabiliwa na malalamiko na radiamali kali kutoka kwa Wapalestina.

1058210
captcha