IQNA

Hafla ya 'Kufarijika na Qur'ani' yafanyika katika Taasisi ya Mawasiliano ya Kiislamu

17:43 - July 23, 2012
Habari ID: 2375758
Hafla ya Kufarijika na Qur'ani' ambayo imewajumuisha makari na mahafidh wa Qur'ani Tukufu wapatao 77 kutoka nchini Misri imefanyika leo mchana katika Taasisi ya Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran mjini Tehran.
Ujumbe wa makari na mahafidh wa Qur'ani kutoka Misri ambao umealikwa humu nchini na Idara ya Masuala ya Qur'ani ya taasisi hiyo utakuwa humu nchini kwa kipindi cha wiki moja.
Swabir Id, Muhammad al-Husseini na Sayyid Ibrahim Warda, makari mashuhuri wa Misri walipata fursa ya kuwafariji hadhirina kwa visimo vyao vya kuvutia vya Qur'ani Tukufu.
Hatimaye hadhirina waliswali swala za adhuhuri na alasiri kwa uimamu wa Ayatullah Taskhiri. 1060609
captcha