‘Waislamu kuwaalika Wakristo kula futari pamoja katika msikiti huu wa kihistoria ni hatua muhimu sana,’ amesema Diji Obadia Haruna, Mkuu wa Tawi la Vijana katika Jumuiya ya Wakristo Nigeria CAN.
Futari hiyo iliandaliwa Jumamosi kwa mnasaba wa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na ilihudhuriwa na vijana 100 Wakristo pamoja na viongozi wao.
Kikao hicho kiliandaliwa na Jumuiya ya Amani ya Waislamu na Wakristo nchini Nigeria chini ya uenyekiti wa Dtk. Suleiman Shuabu Shinkafi.
Inatazamiwa kuwa vikao kama hivyo vya pamoja vitasaidia katika kujenga maelewano, amani na kustahimiliana Waislamu na Wakristo nchini Nigeria.
Katika miezi ya hivi karibuni nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika imeshuhudia machafuko ya kidini ambayo yamepeleka watu wengi kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa
1061122