Gazeti la al Nahar al Jadid linalochapishwa Algeria limeripoti kuwa mashindano hayo yataanza tarehe 20 Ramadhani yakiwashirikisha washindani kutoka nchi 45 na kwamba yatafunguliwa na rais wa nchi hiyo.
Mkurugenzi wa masuala ya Qur’ani katika Wizara ya Masuala ya Kidini na Wakfu ya Algeria Muhannad Edin amesema kuwa mashindano hayo ya Qur’ani yalikuwa yakifanyika kieneo na kwamba sasa yanafanyika katika upeo wa kimataifa.
Muhannad Edin amesemaWizara hiyo imepanua zaidi mashindano hayo na sasa yatashirikisha nchi za mashariki na magharibi mwa dunia kama Indonesia, Ufilipino, America ya Kusini, nchi za Ulaya na Afrika.
Ameongeza kuwa kamati ya majaji wa mashindano hayo itajumuisha majaji wa kimataifa wa Algeria, Jordan na Senegal. 1064936