Taarifa hiyo imetolewa siku mbili tu baada ya kundi la Kiislamu la Islah kuitaka serikali ya nchi hiyo iwaachilie huru wanachama wake waliotiwa nguvuni hivi karibuni.
Taarifa hiyo imewataka watawala wa Imarati wawaachilie huru mara moja wanaharakati hao 50 au kwa uchache wawafungulie mashtaka mahakamani. Imewataka wasimamishe mara moja ukandamizaji wao dhidi ya wapinzani wa kisiasa na kutangaza wazi sehemu walikofungwa wanaharakati wa kisiasa 35 wa nchi hiyo.
Shirika la Msamaha Duniani limeendelea kusema kuwa licha ya kupita miezi kadhaa tokea wapinzani 50 wa nchi hiyo, wengi wao wakiwa ni Waislamu, watiwe nguvuni hadi sasa hakuna mashtaka yoyote ambayo yamewasilishwa dhidi yao mahakamani.
Kundi la Islah ambalo linafungamana na Harakati ya Ikwanul Muslimin limewataka watawala wa Imarati wasimamishe mara moja ukandamizaji na vitisho dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa. Watawala hao waliwatia nguvuni wapinzani hao kwa kisingizio cha kuvuruga nidhamu na utaratibu wa kijamii. 1068519