Akizungumzia suala hilo Adnan Shadhr an-Nassiri mkuu wa Darul Qur'ani ya mji wa Nassiriya amesema matangazo ya redio hiyo yamekuwa yakipeperushwa hewani kwa majaribio kwa muda wa miezi mitatu.
Yahya an-Nassiri, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Upashaji Habari ya Nassiriya amesema redio hiyo ni ya kwana kuasisiwa katika aneo hilo kwa madhumuni ya kutagaza vipindi vya Qur'ani Tukufu na visomo vya Qur'ani kwa mbinu za kitaalamu.
Amesema redio hiyo itakuwa ikipeperusha hewani matangano yake kupitia mawimbi ya FM. Wasimamizi wa redio hiyo wanasema lengo la kuanzishwa kwake ni kueneza maarifa ya Qr'ani Tukufu kupitia visomo tofauti vya Qur'ani, hotuba za tafsiri za Qur'ani pamoja na habari na shughuli tofauti zinazofanyika kitaifa kieneo na kimataifa kuhusiana na kitabu hicho cha wahyi wa Mwenyezi Mungu.
Idhaa hiyo itakuwa ikitangaza vipindi vyake kwa muda wa masaa 17 ambapo itakuwa ikifunguliwa kila siku saa 12 na nusu. 1069478