Kituo hicho cha haki za binadamu kimemtaja kijana aliyeuawa kuwa ni, Hussein Yusuf Al Qallaf mkazi wa eneo la Al Mashari linalopatikana katika mji huo wa Qatif na kwamba aliuawa jana usiku kwa kupigwa risasi na vikosi vya utawala wa Aal Saudi.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa, vikosi vya Saudia viliwavamia raia waliokuwa wanaandamana na kuanza kuwafyatulia risasi hai ambapo mbali na kijana huyo kuuawa wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Aidha vikosi hivyo vya utawala wa Aal Saudi vimewazuia majeruhi kupelekwa katika vituo vya matibabu.
Katika siku za hivi karibuni, mbali na miji ya mashariki ya Qatif na Awwamiyya, miji ya Madina na Riyadh ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo na makao ya wana wa kifalme wa Aal Saudi, imekumbwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala wa nchi hiyo.
1069407