IQNA

Waislamu Ufaransa wanataka chakula halali

18:04 - August 06, 2012
Habari ID: 2387038
Katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, idadi ya Waislamu wanaotaka chakula halali nchini Ufaransa imeongezeka.
Katika kitongoji cha Paris cha Livry Gargan, maduka yanajitahidi kukidhi mahitaji ya chakula halali.
Fatima Assani mwanamke mwenye umri wa miaka 39 mwenye asili ya Morocco ambaye ana watoto wawili anasema yeye hutengeneza supu maalumu mwezi wa Ramadhani na huhakikisha kuwa anatumia bidhaa halali.
Kama Assani, aghalabu ya Waislamu takribani million tano Ufaransa wanachagua vyakula halali. Inakadiriwa kuwa soko la vyakula halali linastawi kwa asilimia 10-15 kwa mwaka. Katika mwezi wa Ramadhani, soko la bidhaa halali linaghariamiwa kupindukia dola milioni 430.
Mapema mwaka huu wanasiasa wenye chuki dhidi ya Uislamu waliibua utata kuhusu vyakula halali. Mwanasiasa wa mrengo wa kulia mwenye misimamo mikali Marine le Pen alikosoa namna Waislamu wanavyochinja.
Pamoja na kuwepo njama kama hizo lakini soko la bidhaa halali limeimarika Ufaransa.
1071633
captcha