Hayo yalisemwa jana Ijumaa na Askofu Beshara Rai huko katika mji wa Akkar. Ameongeza kuwa Wakristo wa Lebanon na Mashariki ya Kati nzima wana jukumu la kuwabainishia Wamagharibi ambao kimsingi huituhumu dini Tukufu ya Kiislamu kwa kuhusika na vitendo vya mabavu, mafundisho ya amani ya dini hii tukufu ili wapate kuifahamu vyema.
Askofu Rai amesema Waislamu pia wanapasa kuiarifisha ulimwenguni dini ya Kikristo kuwa ni dini ya baraka na mazungumzo. Amesisitiza kwamba Ukristo hautokani na Vita vya Msalaba wala ukoloni na kwamba Walebanon wanapasa kuhubiri ujumbe wa amani na upendo wa dini mbili hizi.
Ameongeza kuwa Lebanon ambayo ina wafuasi wengi wa dini mbili hizi haiwezi kupuuza moja ya dini hizo. Vilevile amelitaka jeshi, wanasiasa na viongozi wa kidini wa nchi hiyo kuzingatia juhudi ambazo zinafanywa nchini kwa lengo la kuimarisha usalama wa nchi hiyo. 1081504