Zaidi ya Wairani 75000 watashiriki katika ibada ya Hija mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, safari za ndege za Hija zimeanza Septemba 24 na kila siku mahujaji 3000 watasafirishwa kuelekea Madina na Jeddah.
Kinyume na miaka ya huko nyuma, Mahujaji wa Iran watasafirishwa kupitia Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wakati huo huo mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija amesema, kuanzia wiki ijayo kutakuwa na mikutano ya Mahujaji katika miji mitakatifu ya Madina na Makka kuhusu masuala mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu, mwamko wa Kiislamu, Palestina na wanawake Waislamu.
Ibada ya Hija ni nguzo muhimu ya Uislamu na ni kongamano kubwa zaidi la Waislamu kutoka kona zote za dunia.
1110965