IQNA

13:10 - November 12, 2012
Habari ID: 2446890

Utawala wa Kizayuni washadidisha hujuma Ghaza

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amesema katika kikao cha baraza la mawaziri la utawala huo kuwa Israel imejiandaa kufanya mashambulizi makubwa huko Ghaza.

Utawala ghasibu wa Kizayuni unaokaribia kuandaa uchaguzi wa bunge umegeuza Ghaza kuwa uwanja wa propaganda na mashindano ya wanasiasa wa Israel wanaopigania ushindi kwenye uchaguzi huo.
Karibu Wapalestina kumi wameuliwa shahidi na wengine zaidi ya arubaini kujeruhiwa katika duru mpya ya mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
Ashraf al Qudra Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina ameeleza kuwa, raia wa Palestina wamesababishiwa hasara na maafa katika mashambulizi hayo yaliyo dhidi ya ubinadamu yaliyofanywa na jeshi la Israel usiku wa Jumamosi hadi alfajiri ya Jumapili hii katika maeneo ya kaskazini, mashariki na kusini mwa Ukanda wa Ghaza. Swali muhimu linaloulizwa hapa ni hili kuwa je, ni lengo gani ambalo limewafanya Wazayuni kutekeleza mashambulizi makubwa mara hii huko Ghaza. Utawala wa Kizayuni unaendesha mashambulizi hayo huko Ghaza ili kuwatia mashinikizo viongozi wa harakati ya Hamas na kupotosha fikra za waliowengi ndani ya Israel kuhusu hali ya mambo inayotawala katika utawala huo hivi sasa. Ni wazi kuwa kusimama kidete Hamas katika Ukanda wa Ghaza katika hali ambayo karibu miaka sita inapita sasa tangu utawala haramu wa Kizayuni uwawekee wakazi wa eneo hilo vikwazo vya pande zote, pia kumeulazimisha utawala huo na waungaji mkono wake wa Magharibi kufuata njia nyingine ngumu hasa ikizingatiwa kwamba jitihada za kidiplomasia za kuishawishi harakati ya Hamas iweke kando muqawama hazijazaa matunda. Pamoja na kupita miaka kadhaa ya kukabiliwa na umasikini na mauaji huko Ghaza, eneo hilo lenye watu wengi bado liko chini ya mzingiro wa kiuchumi wa Israel huku likikabiliwa na mashambulizi ya anga na vifaru ya utawala wa Kizayuni kila uchao. Ukanda wa Ghaza umezingirwa tangu mwaka 2007 na hatua ya kusimama kidete wakazi wa eneo hilo mbele ya mzingiro huo wa kiuchumi na mashambulizi ya mara kwa mara ya jeshi la utawala wa Kizayuni imewatia moyo zaidi wa kushikamana bega kwa bega raia hao mbele ya dhulma na ukandamizaji wa maghasibu wa Kizayuni. Eneo la Ukanda wa Ghaza linawanyima usingizi viongozi wa utawala wa Kizayuni licha ya udogo wake wa kilomita mraba 365. Kwa hivyo Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amemaua kuanzisha mchezo mpya dhidi ya Ghaza katika muda wa miezi miwili iliyosalia ya uwaziri mkuu wake lengo lake kuu likiwa ni kuzusha wimbi la uchupaji mipaka dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo na hivyo kuweza kujidhaminia kura za uchaguzi ujao wa mwezi Januari mwakani na wakati huohuo kufunika matatizo yanayoendelea ndani ya utawala huo.
1135083
captcha