Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani haitaki kuona amani na uthabiti vikitawala nchini Syria, bali inataka kuona vita vikiendelea vita vya msugano nchini humo.
Akihutubia kwenye mahafali ya 23 ya kuhitimu wanachuo mjini Beirut, Sayyid Hasssan Nasrullah amesema kuwa, hivi sasa hali ni tata nchini Syria na kwamba, mtu yeyote anayefikiri kwamba wapinzani na waasi wanaweza kuidhibiti hali iliyopo nchini humo anajidanganya. Ameongeza kuwa, kile kinachojiri nchini Syria ni mapigano kati ya wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na wananchi dhidi ya waasi na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na madola ya Magharibi na hasa Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, waasi nchini humo wametenda na wanaendelea kutenda jinai kubwa kwa kuwarusha watu kutoka maghorofani hadi chini na kuwamiminia risasi wananchi wasio na hatia yoyote. Sayyid Nasrullah amebainisha kuwa, mtu yeyote anayekataa kufanya mazungumzo ya kisiasa nchini Syria ni mtenda jinai.
1155147