IQNA

Ujumbe wa Imam Khamenei kwa wanachuo

11:35 - January 14, 2013
Habari ID: 2479856
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, vijana azizi wa taifa la Iran wanapaswa kujiweka tayari kwa ajili ya kupiga hatua zenye kasi kubwa za maendeleo kuelekea kwenye malengo matukufu yaliyoainishwa.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika ujumbe wake kwa mkutano wa 47 wa kila mwaka wa Umoja wa Jumuiya za Wanachuo Waislamu wa Barani Ulaya na kuongeza kuwa, vijana na wana azizi wa taifa la Iran popote walipo duniani wanapaswa kujiweka tayari kutekeleza majukumu yao katika kuongoza nchi yao na kupiga hatua kubwa zenye kasi kubwa kuelekea kwenye malengo matukufu yaliyoainishwa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Iran ya kesho iliyojaa utajiri wa hazina kubwa za kielimu na kivitendo inapaswa iongozwe na viongozi wakubwa wenye ustahiki na kwamba vijana wanapaswa kujipamba kwa sifa za imani, hima, ushujaa na muono wa mbali kwa ajili ya kupiga hatua kubwa na zenye kasi kubwa kuelekea kwenye malengo yaliyoainishwa.

Umoja wa Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu Barani Ulaya una historia ya miaka 47 na ni moja ya jumuiya zilizotoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya ufalme wa Shah nchini Iran na imekuwa muungaji mkono mkubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
1170916
captcha