IQNA

M'bala: Hollywood ni tawi la jeshi la Marekani na Uzayuni

9:40 - February 05, 2013
Habari ID: 2491613
Mcheza tamthilia za kuchekesha wa Ufaransa Dieudonné M'bala M'bala amesema kuwa sekta ya utengenezaji filamu ya Marekani Hollywood ni tawi lisilokuwa la kijeshi la jeshi la Marekani na Uzayuni linalofanya kazi ya kueneza uongo na kudhihirisha mambo yalisiyokuwa na uhakika wowote.
Msanii huyo anayepigania uhuru na kupinga Uzayuni wa Ufaransa ameiambia IQNA kuwa Hollywood ni tawi la jeshi la Marekani na Uzayuni na chombo cha kuhalalisha uongo na kuudhihrisha kuwa ni kweli. M'bala amesema kuwa sekta ya utengenezaji filamu ya Marekani imekuwa parapanda la utawala ghasibu wa Israel na inatumia uwezo wake mkubwa wa kifedha kwa ajili ya kulinda maslahi ya utawala huo.
Amesema filamu za Hollywood zinawaarifisha Waislamu kuwa ni watu wenye fikra finyu, wanaopinga maendeleo na magaidi ili kwa njia hiyo iweze kuchafua sura ya Uislamu ambayo ndiyo adui mkuu wa Uzayuni duniani.
Dieudonné M'bala M'bala amesem kuwa filamu na tamthilia zake zimesusiwa na kumbi nyingi za Ufaransa na pia vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na Uzayuni baada ya kuonesha mchezo unaokosoa uvamizi wa Israel dhidi ya ardhi ya Palestina. 1182929
captcha