Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kundi la kibaguzi linaloongozwa na Den Saxon wiki iliyopita lilikusanyika mbele ya msikiti huo na kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kurarua kurasa zake.
Kiongozi wa kundi hilo, Saxon pia alitoa matamshi ya kifidhuli akisema kuwa kitendo hicho ni haki yao ya uhuru wa kujieleza. Matamshi ya Saxon ambaye ni maarufu kwa misimamo yake ya kibaguzi na kupiga vita Uislamu, yalikabiliwa na upinzani mkali wa wanafunzi wa chuo kikuu cha mji huo.
Siku kadhaa baada ya tukio hilo, viongozi wa dini tofauti wamekusanyika katika Kituo cha Kiislamu na Msikiti wa mji wa Tempe huko Arizona wakilaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu. Viongozi hao wa dini tofauti walishiriki katika shughuli iliyopewa jina la Milango Wazi ya Misikiti na kueleza mshikamano wao na Waislamu wa mji huo.../EM