IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Dubai yaanza

20:36 - June 24, 2015
Habari ID: 3318398
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Dubai yameanza Jumatano hii usiku katika mji huo wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mashindano hayo ambayo pia hujulikana kama Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai mwaka huu yanajumuisha washiriki 80 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbali mbali za Kiarabu, Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu.
Wawakilishi wa  Indonesia, Sudan, Oman, Ivory Coast, Tajikistan and Burkina Faso ndio waliofungua mashindano hayo leo usiku.
Kwa mujibu wa Ebrahim Bu Melha, mkuu wa kamati andalizi, mwaka huu kutatumika program maalumu ya kompyuta kuwapatia pointi washiriki.
Mohammad Hossein Behzadfar ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 alishika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya mabarobaro nchini Iran mwaka jana.
Awamu ya 19 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Dubai  yataendelea kwa muda wa siku 21. Mbali na mashindano ya Qur'ani kutakuwepo pia na mihadhara ya kidni kwa lugha mbali mbali. Mashindano hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Idara ya Biashara na Viwanda mjini Dubai.
Mshindi  wa mashindano hayo atapata zawadi ya fedha taslimu Dirhamu za Dubai, Dh 250,000, wa pili atapata Dh200,000 na watatu Dh150,000.../mh

3318050

captcha